Kwa muda wa miaka minne, mradi wa FoodLAND umekua ukifanya kila juhudi kuzungumzia suala la utapiamlo kwa nchi sita za Kiafrika, ndani ya Afrika Kaskazini na Afrika ya Kati, zikiwemo; Morocco, Tunisia, Uhabeshi, Kenya, Uganda na Tanzania. Mradi huu unanuia kuangazia suala la lishe kwa ujumla na upana kupitia mapendekezo ambayo yanafaa na yanawezekana kutekelezwa ili kupambana na aina mbali mbali za utapiamlo ambazo zimeanea kwa kila nchi, hatma ya mradi huu ni kujitahidi kuchangia kwa kutimia kwa malengo endelevu ya maendeleo, haswa lengo la pili nukta mbili ambalo linanuia kupunguza kwa kiasi kikubwa aina zote za utapiamlo.
Miongo mingi ya kubalika kwa mifumo ya chakula kumechangia pakubwa viwango vya utapiamlo ikijumuishwa pamoja na mambo kama kudumaa na kuongezeka kwa kiwango kikubwa kwa fetma na uzito kupita kiasi. Kwa kila mojawapo ya nchi za Kiafrika changamoto hizi hujidhihirisha kwa aina ya kipekee, Kwa sasa Kenya inapambana na mzigo wa pande tatu za utapiamlo, zikiwemo kutokua na lishe bora ya kutosha, lishe kupita kiasi na upungufu wa madini muhimu mwilini. Ni dhahiri na wazi kwamba viwango vya kutokua na lishe bora ya kutosha vinapungua ilihali viwango vya lishe kupita kiasi vinaongezeka kwa vikundi mbali mbali nchini hata ingawa nchi tofauti huonyesha viwango tofauti vya utapiamlo.
Mitindo hii husititiza umuhimu wa kupanga kwa haraka ugavi wa chakula unaolenga lishe bora, haswa kuhakikisha upatikanaji na uwezo wa kununua vyakula vyenye lishe bora kwa watu waliomo kwenye mazingira magumu kama watoto na akina mama. Kwa uhakika uchanganuzi wa viwango na hali ya chakula nchini Kenya umeonyesha changamoto kama vile asilimia sitini (60%) tu ya watoto wanaozaliwa ndio huweza kunyonyeshwa na mara ambayo hufanyika inatofautiana na lishe ya watoto. Hata ingawa viwango vya kudumaa, fetma na kuongezeka kwa uzito kupita kiasi vimepungua bado kuna changamoto mingi kwa watu wenye umri mdogo. Miongoni mwa vijana, wavulana wako na uwezo kubwa kuwa na uzito kiasi kuliko wasichana nao wasichana wakiwa na uzito kupita kiasi kuliko wavulana.
Mapendekezo ya lishe yaliyowasilishwa na FoodLAND yanalenga kuziba pengo lililo kati ya tabia ya chakula zilizomo na lishe inayohitajika. Kundi lililokua linapatiana mapendekezo lilitumia njia tatu muhimu za kupata mapendekezo haya. moja ikiwa ni ukaguzi wa kina uliozingatia fasihi ya kisayansi. Pili ikiwa ni utafiti uliofanyika mjini na vijijini, ukizingatia kwa makini wanawake na watoto chini ya siku zao elfu (1000) za kwanza. Tatu pembejeo kutoka kwa washikadau muhimu wa utapiamlo wanaohusika kuthibitisha mapendekezo yaliyotolewa na kuona zile pengo zilizo kwenye mapendekezo ili kuzijaza.
Mapendekezo maalum kwa wanaume na wanawake na vikundi vya umri tofauti
Wataalam wa lishe kutoka FoodLAND walitoa mapendekezo 121 kwa ujumla ya lishe bora kwa Kenya, iliyopendekezwa kwa vikundi maalum ndani ya mizinguko ya maisha tofauti na pia yakizingatia mahitaji tofauti ya mlo ambao wanawake na wanaume waliobalehe wanahitaji.
Ndani ya muktadha wa Kenya, serikali kupitia wizara ya afya imeunganisha wizara zingine, na kuweka mikakati ya kuboresha afya kupitia njia tofauti zikiwemo, miswada, elimu kwenye vituo za afya, huduma za afya na shughuli za mafunzo. Wataalam walizangatia mambo haya walipokua wanatengeneza mapendekezo, wakiweka wizara ya afya kutekeleza baadhi ya haya mapendekezo. Mapendekezo mengine yanashughulikiwa na watumiaji na wanaotengeneza vyakula. foodland.uonbi.ac.ke